Mabadiliko kwenye kikosi cha Azam FC yameendelea kutokea ambapo sasa yamewapa nafasi wachezaji Samih Haji Nuhu na Jabir Aziz kuingia kwenye kikosi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Toto Afrika itakayochezwa kwesho kwenye uwanja wa Uhuru.

Azam FC imetibu ugonjwa wa kufunga baada ya kufunga magoli tisa (9) katika mechi tatu lakini pia ukuta wake umeruhusu magoli manne (4) katika mechi hizo na sasa kocha mkuu wa Azam FC Stewart John Hall analifanyia kazi tatizo hilo la kuruhusu magoli akitaka clean sheets.

Jabir Aziz ambaye kiasili ni kiungo mkabaji ambaye amekuwa hakosekani kwenye kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars amekuwa akikalia benchi kwa muda mrefu pale azam FC hadi mechi iliyopita ambapo Stewart Hall alimpanga wing ya kushoto lakini baadaye alipomtoa Salum Abubakar na Jabir kwenda kucheza Dimba la kati Stewart Hall aligundua mambo mengi aliyonayo kinda huyu na tiba ya kujisahau na umakini katika kukaba kwa timu.

Licha ya kuwepo nyota kama Selemani Kassim na Jamal Myate ambao kocha Stewart anawakubali sana, Leo anatarajia pia kumchezesha Haji Nuhu upande wa winga ya kushoto. Chipukizi huyu ambaye kocha Stewart Hall anaamini kuwa atakuja kuwa beki bora kabisa wa upande wa kushoto nchini leo atapangwa ili asaidie ulinzi na kuondoa tatizo la ukabaji.

Stewat Hall anasema wachezaji watano (5) kama Redondo, Salum Abubakar, Bocco, Mnyate na Ngassa wanapokuwa uwanjani timu inabaki na wachezaji watano tuu wakabaji na hii ni hatari sana hasa unapocheza na timu ngumu na unapohitaji kuufunga mchezo, ni vizuri kutengeneza timu yenye wachezaji wa aina tofauti ili tuwe na uwezo wa kucheza staili tofauti kulingana na mazingira ya mchezo.

Azam FC katika mechi ya leo itawakosa wachezaji sita (6) Jamal Mnyate, Salum Abubakar, Tumba Swedi, Cosmas Lewis, Daudi Mwaisongole na Himid Mao ambao wapo na timu ya Taif ya Vijana lakini baada ya mechi ya kesho huenda Haji Nuhu akaungana na makinda wenzake timu ya Taifa na kufanya idadi kufikia saba. Haji Nuhu ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na kama kocha wa timu ya Taifa ya Vijana Jamhuri Kihwelu atakuja uwanjani basi bila shaka atamuona Haji.

Mechi ya Kesho itakuwa nafasi nyingine kwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars kumuona tena Ramadhan Chombo Redondo mchezaji ambaye tovuti ya www.azamfc.co.tz inaamini kuwa anafaa kuwemo kwenye kikosi cha Stars sambamba na John Bocco na Erasto Nyoni.

Azam FC kesho inatarajiwa kuwakilishwa kama ifuatavyo

 1. Vladmir Niyonkuru Azam One
 2. Ibrahim Shikanda Mungiki
 3. Mutesa Patrick Mafisango Pedejee
 4. Aggrey Morris Chacha
 5. Erasto Nyoni Machine
 6. Ibrahim Mwaipopo Popoz
 7. Mrisho Ngasa Uncle
 8. Jabir Aziz Stima
 9. John Bocco Adebagoals
 10. Ramadhan Chombo Redondo
 11. Samih Haji Nuhu