Kesho jioni kwenye uwanja wa Uhuru Azam FC itashuka dimbani kujaribu mbinu zake na pasi zake mpya zilizoletwa na kocha mpya Stewart Hall. Mechi ya kesho inafuatia mechi iliyoacha historia mpya kwenye uwanja wa Taifa jumapili iliyopita baada ya Azam FC kuipeleka puta Simba SC.

Azam FC ambayo sasa inatumia kiwanja chake cha mazoezi cha kule Chamazi imefanya badiliko moja tuu kwenye kikosi chake. Jabir Aziz Stima ambaye alikuwa anasumbuliwa na maumivu aliyorudi nayo Misri ambako alikwenda kuiwakilisha timu ya taifa Taifa Stars kesho ataanza kuchukua nafasi ya kinda Jamal Mnyate ambaye aling'ara sana siku Azam FC inaisasambua Simba SC.

Kwa ujumla kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo

1. Vladmir Niyonkuru

2. Ibrahim Shikanda

3. Mutesa Patrick Mafisango

4. Aggrey Morris

5. Erasto Nyoni

6. Ibrahim Mwaipopo

7. Mrisho Ngasa

8. Salum Abubakar

9. John Bocco

10. Ramadhan Chombo

11. Jabir Aziz