Timu ya Azam FC siku ya Jumapili itashuka dimbani kukabiliana na Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, timu ya Simba SC katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu, utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .

 

Mchezo wa kesho utakuwa wa pili kwa upande wa Azam FC ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, wakati Simba SC itakuwa ikicheza mchezo wake wa kwanza kwa mzunguko huu wa lala salama.

 

Azam FC imekamilisha maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo ikiwa kambini na kutumia uwanja wao wa nyumbani kwaajili ya mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo pamoja na michezo mingine.

 

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa uwanja wa Mkwakwani, mkoani Tanga Azam FC ikiwa nyumbani ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa 2-0 na timu hiyo (Simba).

 

Mchezo wa kesho dhidi ya Simba utakuwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu kuchezwa uwanja wa Taifa unaohusisha timu mbali ya Simba na Yanga, Azam FC imepata fursa ya kuchezea uwanja huo ikiwa ni moja ya timu inayojipatia wapenzi kadri muda unavyokwenda na kuongeza ushindani katika ligi kuu ya Vodacom.

 

Azam FC inatakiwa kushinda mchezo huo ili kujiweka vizuri katika nafasi nzuri katika, itatumia wachezaji wake waliokuwa katika timu ya Taifa ambao ni Mrisho Ngassa, Jabir Aziz na Aggrey Moris.

 

 

Azam FC yafanya mabadiliko ya uongozi, wametoka Kondo, Jeshi na King.

 

Uongozi wa Azam FC umefikia makubaliano ya kuwatoa  katika nafasi zao kocha msaidizi Habib Kondo, meneja Ibrahim Jeshi na mwekahazina Mohamed Seif ‘King’ kwa manufaa ya klabu.

 

Makubaliano hayo yamefikia mwanzoni mwa wiki hii kwa dhumuni la kuleta mabadiliko ya uongozi ili kuboresha timu hiyo.

 

Akizungumza na tovuti ya www.azamfc.co.tz, Katibu  Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa alisema wamefikia uamuzi huo ili kupisha taratibu zingine zitakazofuata kukuza klabu hiyo.

 

“tumewatoa katika nafasi zao lakini bado ni wafanyakazi wa kampuni yetu, tumefikia makubaliano hayo ili kuleta mabadiliko ambayo tunaamini yatatusaidia katika kukuza na kuendeleza klabu yetu” alisema Idrissa.

 

Alisema pamoja na kuwatoa viongozi hao timu itaendelea kufanya kazi zake za kawaida ikiwa ni pamoja na mazoezi yanayosimamiwa na kocha Stewart Hall, pamoja na kocha Idd Aboubakar.

 

Naye kocha Stewart alisema kuziba nafasi ya kocha aliyeondoka kwa sasa atamtumia mchezaji Kally Ongala kuwa kama kocha mchezaji ambaye atakuwa akisaidiana nae kutoa maelekezo ya kukifundisha kikosi hicho.

 

“Kocha ameondoka, namtumia Kally kunisaidia kutoa maelekezo kwa wachezaji wengine, anaouwezo wa kufanya hivyo, pia ameonyesha juhudi zake binafsi kuhakikisha wachezaji wanaelewa na kufuata maelekezo yote” alisema Stewart.

 

Kally kwa nafasi yake alisema anashukuru kupatiwa nafasi hiyo, anaitumia nafasi hiyo kama