Kesho katika uwanja mkuu wa Taifa kutakuwa na burudani ya kukata na shoka, Ni mchezo kati ya Timu ya zamani (Simba SC) na timu ya kisasa (Azam FC), ni mchezo kati ya Football Fitna na Football Science, ni mchezo kati ya wapenda mabadiliko na wapinga mabadiliko, ni mchezo kati ya soka la kisasa na soka la kizamani, ni mchezo kati ya mfumo mpya kwenye football na mfumo wa kizamani. Ni kati ya Azam FC na Simba SC.

Mchezo wa kesho utakuwa wa ukipima mbinu za Mzambia Patrick Phiri ambaye anaaminika kuwa ndiye kocha bora kabisa kwa sasa nchini na kocha mpya wa Azam FC Stewart John Hall ambaye amekuja kumpa changamoto Patrick Phili. Makocha hawa wawili ni marafiki na kila mmoja anamkubali mwenzake. Stewart Hall anaamini kuwa Phiri ndiye kocha mwenye uwezo zaidi ya makocha wote ligi kuu ya Tanzania na ufundishaji wake unazingatia ueledi. Phiri kwa upande wake naye  anaamini kuwa muingereza wa Azam ana mbinu, elimu na uzoefu mkubwa utakaowawezesha Azam FC kutamba kwenye siku za usoni kama ilivyo kwa Phiri.

Makocha hawa wawili wamekuwa wakikutana na wakati mwingine kufanya mazoezi pamoja uwanja wa Uhuru kabla ya Azam FC kuhamia kwenye kiwanja chake kule Chamazi.

Mchezo wa kesho utakuwa ukipima ubora wa mifumo kati ya 4-4-2 wa Simba SC na 4-3-3 wa Azam FC.

Simba inatarajiwa kuwakilishwa na wachezaji wafuatao

Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah, Juma Nyoso, Meshak Abel, Jerry Santo, Mohammed Banka, Patrick Ochan, Mussa Hassan Mgosi, Mbwana Samata na Rashid Chiddy Gumbo. Kikosi cha Azam FC kitakachoanza kesho kitawekwa hadharani kwenye facebook

Akizungumzia mchezo wa kesho, kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall amesema, ni mchezo wa kawaida wa ligi kuu, kama tuliweza kufungwa na Kagera Tanga basi tunaweza kufungwa na Simba SC lakini kama tuliweza kuifunga Mtibwa Sugar 4-0 Manungu pia tunaweza kuifunga Simba SC. Ndiyo Simba ni timu bingwa na kubwa lakini pia sisi ni timu kubwa na tuna wachezaji wenye uwezo wa kufanya maajabu. Muhimu ni kuwa makini wakati wote wa mchezo. Tukifanya makosa tutafungwa kwa hiyo tunapaswa kupunguza makosa ya kipuuzi.

Asubuhi ya Leo Mtandao wa Azam FC umezungumza na afisa habari wa Simba SC nay eye amethibitisha kuwa mechi ya kesho itachezwa kwenye uwanja mpya mkubwa wa Taifa  kwa hiyo mashabiki wa Azam FC mjiandae kuja kuishangilia timu yenu.

Manahodha wote wawili wa Azam FC Ibrahim Shikanda na Aggrey Morris wameahidi kucheza kufa na kupona kuhakikisha tunapata pointi tatu na kurejesha ndoto zetu za kucheza mashindano ya kimataifa mwakani.

Mtandao wa Azam FC www.azamfc.co.tz unaamini kuwa hakuna sababu itakayotuzuia kuvuna pointi zote tatu hiyo kesho.