Azam FC leo itashuka uwanja wa Amaan kukabiliana na timu ngumu ya Zanzibar Ocean View katika mchezo wao wa pili wa mashindano yanayoendelea ya Kombe la Mapinduzi.

 

Azam FC wataingia uwanjani majira ya saa kumi jioni wakiwa na pointi tatu huku Ocean View itakuwa na pointi moja baada ya kutoka sare na katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Yanga.

 

Mchezo huo unakutanisha timu zinazomilikiwa na wafanyabiashara maarufu katika kanda zote Zanzibar na Tanzania Bara, Azam FC inamilikiwa na mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na Kati Said Salim Bakhresa ambaye ni Mzanzibari huku Ocean View ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa kutoka Zanzibar Ibrahim Makungu.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wa kasi kwa timu zote kwani, timu hizo zinaundwa na wachezaji wenye viwango vya juu na uwezo wawapo uwanjani kuliko timu yoyote iliyokatika kundi lao.

 

Mechi nyingine itafanyika usiku wa saa mbili usiku ambapo Yanga watacheza na timu inayochipukia ya Chuoni.