Tangu aondoke Itamar Amorin Azam FC imefikisha mchezo wa tano ikishinda michezo yote mitano mfululizo, mmoja ukiwa ni ya ligi na minne ikiwa ni ya kirafiki na timu za ligi kuu za Simba, Yanga, AFC Leopards ya Kenya na African Lyon.

Azam FC iliifunga Ruvu Shooting 4-1, Ikaifunga Simba 3-2, Ikaifunga Yanga 3-1, Ikaifunga African Lyon 2-1 na jana Imeifunga AFC Leopards toka ligi kuu ya kenya 4-0

Katika mchezo uliochezwa jana jioni timu ya soka ya FC Leopards ya Kenya imeendeleza wimbi la kupoteza michezo yake ya kirafiki jijini Dar es Salaam baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Uhuru.

 

Katika mchezo huo ambao Azam FC waliutawala kwa asilimia 100 na kuufanya wa upande mmoja kwa Azam FC kutawala dakika zote 90;

 

Azam walinza kujiandikia bao kwanza dakika ya 7 likipachikwa na John Bocco ‘Adebayor’ baada ya kuunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.

 

Azam waliendelea kulishambulia lango la Leopards kwa nguvu na kama washambuliaji wake wangekuwa makini, wangeweza kutoka na karamu ya mabao, kabla ya Ngassa kupachika bao la pili dakika ya 42 baada ya kumegewa pande safi na Kali Ongala na kuingia na mpira kwenye box na kuachia shuti lililotinga wavuni.

 

Kipindi cha pili kilianza kwa kishindo ambapo Leopards walikuja juu kutaka kusawazisha mabao hayo lakini wakajikuta wakipachikwa bao la tatu na nne dakika ya 73 na 80 yakifungwa na Mau Bofu na Bocco, hivyo hadi mwisho wa mchezo, Azam FC wakachomoza na ushindi huo mnono wa mabao 4-0.

 

Timu hiyo ya Kenya imemaliza ziara yake hiyo ikipoteza michezo yote baada ya kufungua dimba na Simba na kukandamizwa mabao 2-0, kabla ya kukutana Yanga juzi na kuchezea kichapo cha bao 1-0.

Azam FC; Vadmir Niyonkuru/Jackson Chove, Ibrahim Shikanda, Mau Bofu, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Ibrahim Mwaipopo, Selemani Kassim/Jabir Aziz, Salum Abubakar/Himid Mao, John Bocco, Kally Ongala/Peter Senyonjo na Mrisho Ngasa/Jamal Mnyate