Ikicheza mechi yake ya tatu ya kirafiki baada ya kuho nyuma kuzipa kichapo cha 3-2 na 3-1 Timu Kongwe za Simba na Yanga, Leo asubuhi kwenye uwanja wa Uhuru, Timu ya Azam FC imeifunga African Lyon 2-1.

African Lyon ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata goli kwa njia ya penati mfungaji akiwa ni Zahoro Pazi baada ya kipa wa Azam FC Vladmir Niyonkuru kumuangusha beki Hamis Yusuf.

Azam FC walitulia na kupanga mashambulizi lakini mipira mingi iliishia mikononi mwa kipa mkongwe wa African Lyon Ivo Mapunda.

Viungo wa Azam FC Salum Abubakar na Partick Mafisango leo walionesha kandanda safi sana lakini iliwalazimu Azam FC kusubiri timu ya pili iingie uwanjani kuweza kupata magoli. Viungo waliocheza kipindi cha pili ni Ibrahim Mwaipopo na Jabir Aziz.

Azam FC ilipata goli la kusawazisha baada ya Jamal Mnyate kuwazidi mbio, akili na nguvu walinzi wa AFC na kuukwamisha mpira ndani ya nyavu.

Azam FC ilijipatia goli la pili baada ya Jamal Mnyate tena kuwakimbiza mabeki wa Lyon kisha kupiga krosi iliyounganishwa vema na Peter SSenyonjo.

Hadi mwisho wa mchezo Azam FC 2-1 African Lyon

Azam FC, Vladmir niyonkuru/Jackson Chove, Ibrahim Shikanda/Malika Mdeule, Mau Bofu/Haji Nuhu, Tumba Swedi/Lackson Kakolaki, Erasto Nyoni/Himi Mao, Mutesa Mafisango/Ibrahim Mwaipopo, Ramadhani Chombo/Selemani Kassim Selembe, Salum Abubakar/Jabir Aziz, John Bocco/Peter SSenyonjo, Kally Ongala/Philip Alando, Mrisho Ngasa/Jamal Mnyate