Leo katika uwanja wa Uhuru, Azam FC itaikaribisha AFC Leopards ya Kenya katika mechi ya kimataifa ya kirafiki. AzamFC ambao Siku chache zilizopitz  walipomosha vipigo vyaa 3-1 kwa Yanga, 3-2 Kwa Simba na 2-1 Kwa African Lyon itahitaji kushinda mechi ya leo ili kuendeleza rekodi yake nzuri.

 

Mchezo huo utakaochezwa saa saa kumi jioni utakuwa ni matayarisho kwa ajili ya kujiandaa na kushiriki kombe Mapinduzi, litakaloanza Januari 2-12 visiwani Zanzibar.

 

Kocha mkuu wa klabu hiyo Stewart Hall alisema kabla ya mechi dhidi ya African Lyon kuwa mechi hiyo itakuwa muhimu kwa timu hiyo kupima uwezo wake baada ya kurekebisha baadhi ya makosa yaliyojitokeza mechi iliyopita.

Mzozo: kombe litabaki Azam

Mabingwa watetezi kombe la Uhai, Azam Academy wapo katika maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo inayojuisha timu za vijana za timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom VPL.

 

Uhai Cup 2010 itaanza kurindima Jumatatu Des 27 na kumalizika Jan 10 2011, Azam Academy watafungua dimba na Ruvu Shooting katika mchezo wa pili wa mashindano hayo yatakayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

 

Akiongea na tovuti ya azamfc.co.tz, kocha Mkuu wa Azam Academy Herry Mzozo amesema wachezaji wote wapo katika maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo akiamini mwaka huu yatakuwa magumu na yenye upinzani zaidi ya miaka iliyopita.

 

“Timu shiriki zimejiandaa vizuri, hakuna mashindano rahisi lakini mwaka huu wameonyesha jitahada, wametunza timu zao na kucheza mechi nyingi za majaribio hivyo nasi tunajiandaa zaidi kutetea ubingwa wetu wa miaka miwili mfululizo” amesema Mzozo.

 

Mzozo ameongeza kuwa katika fainali za mwaka huu kikosi hicho kitawakosa wachezaji wake mahiri watano waliopanda kucheza timu ya wakubwa Azam FC, wachezaji hao ni Tumba Swed, Himid Mao, Mau Bofu, Sino Augustino na Haji Nuhu.

 

“tumesajili wachezaji wengine watakaochukua nafasi zao ninauhakika watafanya vizuri katika michezo hiyo na kubakisha kombe nyumbani.”Mzozo.

 

Akizungumzia kundi walilowekwa, kocha huyo mzawa amesema katika mpira hakuna timu ndogo, kila timu inanafasi ya kuifunga timu pinzani hivyo wanaelekeza nguvu kwa timu zote watakazokutana nazo.

 

Azam imepangwa kundi A pamoja na AFC, Polisi Dodoma, Ruvu Shooting na Toto African, kundi B linaundwa na Simba, Yanga, African Lyon na Toto African huku kundi C linajumuisha Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Majimaji FC na JKT Ruvu.

 

Azam wamechukua kombe hilo linalidhaminiwa na kampuni ya Bakhressa BSS kupitia bidhaa ya maji ya Uhai.