Huenda Tanzania ikawa ndiyo nchi yenye mashabiki bora kabisa wa mpira kusini mwa janga la Sahara. Mashabiki wengi wa Tanzania wamegawanyika katika makundi mawili, Simba na Yanga. Nawaita mashabiki bora kwa kuwa unapocheza na moja ya timu hizi kama una timu nzuri na umejiandaa tarajia kupata sapoti toka upande wa pili.

 

Wiki chache zilizopita tulicheza na Simba na kuifunga 3-2. Mashabiki wa Yanga walitupa sapoti kubwa sana na leo tumecheza na Yanga na kuwafunga 3-1 mashabiki wa Simba walikuwa bega kwa bega nasisi.

 

Kumbe unachotakiwa ni kushinda tuu. Ukishinda mechi unapata mashabiki. Hili linatia moyo sana

 

Leo katika uwanja wa Uhuru kulichezwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Azam FC na Azam FC kuibuka wa shindi kwa kuisasambua Yanga 3-1.

 

Mechi hii imechezwa iliwa siku nne tu tangu waanze kufundishwa chini ya kocha mpya Stewart Hall, timu ya Azam FC imepata ushindi wa 3-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Mchezo huo wa pili wa kirafiki kwa Azam baada ya kuwafunga watani wa jadi wa Yanga, timu ya Simba SC 3-2 kwenye mchezo uliochezwa mwezi uliopita uwanjani hapo.

 

Katika mchezo wa leo licha ya kupata ushindi lakini Azam FC wamenifanya nisijutie muda wangu na petroli yangu kwenda uwanjani. Petroli imepanda bei, unapoamua kuwasha gari kwenda uwanjani kuangalia mpira lazima uone mpira, ufurahi na uridhike. Kama timu inacheza mpira mbovu mashabiki hawawezi kwenda uwanjani ilikuwa kauli ya kocha wa Azam FC Stewart John Hall alipoongea nami kwa simu muda mchache baada ya mechi kumalizika.

 

Mshambuliaji mahiri wa klabu ya Azam FC, John Bocco aliipatia Azam FC magoli mawili, goli la kwanza katika dakika ya 22 baada ya kutumia vyema uzembe wa mabeki na golikipa wa Yanga Ivan Knezevic na kuandika goli hilo.

 

Bocco alifunga goli la tatu dakika ya 45 akiwa yeye mwenyewe baada ya walinzi wa Yanga walioonekana kusahau kazi yao kumuacha peke yake na kuandika goli hilo.

 

Goli la pili liliwekwa kimiani na kiungo kutoka nchini Rwanda, Mutesa Patrick Mafisango aliyetumia kosa la golikipa Knezevic baada ya mpira kumponyoka na Mafisango kutumia nafasi hiyo kuandika goli la pili.

 

Azam FC wakicheza kwa kuelewana kama kawaida yao na kuonyesha kiwango cha hali ya juu mbele ya mashabiki waliofika uwanjani hapo walitawala mchezo kwa muda mrefu.

 

Yanga kwa nyakati tofauti walitoa mashambulizi machache, dakika za 12 na 15 mshambuliaji Idd Mbaga alikosa magoli ya wazi na kufanya mashabiki wa Yanga kulalamika.

 

Katika mchezo huo Kostadin Papic alifanya mabadiliko kuingiza kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambacho kilibadili mchezo na kupata goli hilo pekee dakika ya 84 kupitia kwa mshambuliaji mpya aliyesajiliwa dirisha dogo Davis Mwape aliyepokea mpira kutoka kwa Jeryson Tegete.

 

Kikosi kazi cha Azam FC kiliundwa na Vladimir Niyonkuru, Malika Ndeule, Mau Bofu/Samer Nuhu, Agrey Moris, Erasto Nyoni, Mutesa Mafisango, Salum Aboubakar, John Bocco/Ally Manzi, Peter Senyonjo ba Seleman Kassim.