Kikosi cha Azam FC kitashuka dimbani siku ya Jumamosi kucheza na Yanga katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Azam FC watashuka katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuwalaza 3-2 watani zao wa jadi Simba SC kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja huohuo.

 

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili ambazo zitashiriki mashondano ya Kombe la Mapinduzi na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.

 

Kocha wa Azam FC Stewart Hall amesema mechi hiyo imekuja mapema sana itachezwa siku yake ya nne akiwa na timu hiyo.

 

“Nimekuta mechi imeshapangwa, tuna kikosi imara ninaamini watafanya vizuri kwani walishaanza mazoezi mapema wiki hii kwaajili ya mchezo huo.” amesema Stewart.

 

Azam FC na Yanga zinacheza mchezo huo wakiwa narekodi ya kutoka sare katika mchezo wao wa ligi kuu katika mzunguko wa kwanza, Yanga wataitumia mechi hiyo kutambulisha wachezaji wake wapya waliosajiliwa dirisha dogo akiwepo Davis Mwape.