Siku mbili baada ya kuanza kuifundisha timu ya Azam FC kocha Stewart Hall amesema ataendea kukuza na kuendeleza soka la vijana kama ilivyo misingi ya klabu hiyo.

 

Akizungumza baada ya kumaliza mazoezi katika Uwanja wa Uhuru kocha amesema kuendeleza vijana ni msingi mkuu katika klabu yoyote inayohitaji maendeleo bila ya kuwa na vijana hakutakuwa na hatua yoyote nzuri.

 

“najua umuhimu wa kukuza vijana wadogo, nitatoa msaada wangu kuhakikisha tunapata wachezaji bora hapo baadae ambao wataunda timu bora ya taifa na kuleta taswira nzuri ya ligi kuu.” amesema Stewart.

 

Ameongeza kuwa atatumia uzoefu wake alioupata akiwa na timu mbalimbali za vijana kusaidia klabu hiyo kufikia malengo ikiwa ni jukumu lake kama kocha mkuu wa klabu hiyo.

 

Katika kutekeleza hilo kocha huyo ameanza mazoezi na wachezaji zaidi ya watatu wa kutoka timu ya Azam Academy, ikiwa ni sehemu ya kuwapa uzoefu wa kucheza mechi za timu kubwa ya Azam FC.

 

Azam FC ina wachezaji wengi vijana wanaounda Azam Academy, wachezaji hao wadogo wamegawanyika katika makundi matatu, wapo U20, U17 na U15 ambao wanafundishwa chini ya kocha Herry Mzozo.

 

Maandalizi kwa ujumla.

 

Kocha mkuu wa Azam FC amesema timu inatakiwa kufanya mazoezi ya haraka ili kwenda sawa na mashindano yanayoikabili kuanzia mwezi ujao.

 

Azam FC imealikwa kushiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi Zanzibar litakaloanza Jan 2-12, huku ligi kuu ya Vodacom VPL duru la pili litaanza kurindima kuanzia Jan 15 mwaka kesho.

 

Kocha Stewart amesema muda uliopo ni mchache kujiandaa na mazoezi yatakayokidhi mahitaji ya kushiriki mashindano hayo na ligi kuu, ili kwenda sawa timu itaanza kufanya mazoezi mara mbili kwa siku.

 

“Tutaongeza mazoezi ya jioni, mazoezi ya asubuhi pekee hayatakamisha maandalizi yote, timu inakabiliwa na mashindano na ligi kuu tukianza mazoezi mara mbili kwa siku tutafikia malengo yetu ya kumaliza program zetu za mazoezi”amesema Stewart.

 

Ameongeza kuwa ataanza programu hiyo baada ya wachezaji waliokuwa katika mashindano ya CECAFA kurejea kutoka mapumziko.

 

“wachezaji wote wakisharejea na kucheza mechi yetu ya kirafiki dhidi ya Yanga nitajua timu inaitaji kitu gani na kurekebisha makosa yatakayooneka”amesema Stewart.

 

 

Wasemavyo kuhusu kocha Stewart.

 

Kondo: tutanufaika na ujio wake

 

Kocha msaidizi wa Azam FC Habib Kondo amesema ujio wa kocha Stewart Hall katika klabu hiyo utawapa nafasi ya kuongeza ujuzi wao kutoka kwa kocha.

 

Kondo amesema kocha Stewart ni zaidi ya kocha ni mkufunzi wa makocha hivyo anaamini uwepo wake katika klabu hiyo utakuwa si kwa manufaa ya klabu tu bali hata kwa waalimu wasaidizi.

 

“tumepata mwalimu mwenye uwezo wa juu anaweza kufundisha wachezaji na makocha, tunategemea kuongeza uzoefu wetu, tunaamini tutanufaika zaidi na mafunzo yake”amesema Kondo.

 

Ameongeza kuwa kocha huyo anahitaji kupewa muda zaidi ili kuisaidia timu kwani amekuja ikiwa bado muda mfupi kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu.

 

“najua watanzania wengi wataitaki kuona akifanya vizuri katika mechi ya kwanza lakini mpira hauko hivyo kocha atakuwa akiwapa mafunzo wachezaji na pindi watakapoelewa zaidi wataanza kufanyavizuri” Kondo.

 

Senyonjo: kocha mzuri

 

Mchezaji wa kulipwa wa Azam FC Peter Senyonjo kutoka Uganda amesema kocha mpya wa klabu Stewart Hall ataleta mabadiliko yatakayopelekea timu hiyokuendelea kufanya vizuri katika mechi zijazo.

 

Senjonjo amesema kocha huyo ameonyesha uwezo wake mzuri kwa kipindi kifupi alichoanza kuifundisha timu hiyo.

 

“Nimemuona katika mazoezi ya jana na leo, ni kocha mzuri anautaratimu unaoeleweka kwa kila mchezaji, akiendelea hivi hivi tutakuwa timu na timu bora itakayozidisha ushindani katika misimu ijayo ya ligi kuu.”amesema Senyonjo.

 

Akizungumzia kitu kikubwa alichokiaona kwa kocha huyo ni mazoezi ya kuongeza kasi kwa wachezaji, mazoezi ambayo muhimu kupewa wachezaji wote yanayojenga timu itakayocheza mchezo wa kasi.

 

Himid Mao: tutafanya vizuri

Mchezaji chipukizi wa Azam FC Himid Mao anaamini kuja kwa kocha Stewart Hall raia wa Uingereza kutaongeza mafanikio kwa timu hiyo.

 

Himid amesema kulingana na mazoezi waliyoanza kufanya toka jana (Jumatano) anauhakika timu itabadilika na kuwa katika mfumo wa kisasa zaidi.

 

“Mafanikio yanaonekana mapema, na kocha mzuri anajulikana mapema, siku chache tulizoanza mazoezi na kocha wetu ametundisha mambo mengi muhimu naamini kabisa tutakuwa wazuri na tishio zaidi.”Himid.

 

Himid amewataka wachezaji wenzake wafuate mafunzo ya mwalimu yatawasaidia kukuza mpira wao na kujenga timu imara.