Timu ya Azam FC ipo katika maandalizi ya kujiweka sawa kushiriki katika kombe la Mapinduzi linalotarajiwa kuanza kufanyika Januari 2-12 visiwani Zanzibar. Kombe hilo linajumuisha timu nne za juu kutoka ligi kuu ya Tanzania bara VPL na ligi kuu ya visiwani humo.

 

Azam FC wako katika mazoezi maalum kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo ikiwa sambamba na kujiweka sawa kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara utakaoanza kutimuavumbi Januari 15.

 

Kocha msaidizi wa klabu hiyo Habib Kondo akizungumza na tovuti ya Azam FC wakiwa mazoezini Uwanja wa Uhuru alisema maandalizi yanakwenda vizuri wachezaji wote wanapata mafunzo kama kawaida.

 

“Mashindano ni mashindano tunaheshimu mashindano yoyote tutakayoshiriki hivyo tunafanya maandalizi mapema ili kuwa na timu nzuri itakayoleta ushindani katika mshindano hayo ambayo ni muhimu kwetu tukiwa ytunajiandaa kumalizi msimu ujao.” alisema Kondo.

 

Akizungumzia mahudhurio ya wachezaji alisema wachezaji wengi wa kigeni wamefika isipokuwa Ibrahim Shikanda wa Kenya anayetarajiwa kuwasili muda wowote, Peter Senyonjo anasumbuliwa na malaria, Kally Ongala amepata tatizo la kifamilia amempoteza baba yake Mzazi Dr Remmy Ongala na wachezaji waliopo Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars bado hawajajiunga na mazoezi.