Kutokana na marekebisho yanayoendelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam , Timu ya Azam FC itaendelea kutumia uwanja wa Mkwakwani katika mzunguko wa pili wa ligi kuu unaotarajiwa kuendelea mwakani.

Akizungumza na tovuti ya Azam FC katibu wa klabu Nassor Idrissa amesema watatumia uwanja huo kwa kuwa Uwanja wa Uhuru bado unamarekebisho mengine hivyo wameelekeza nguvu zao katika kuhakikisha uwanja wa Mkwakwani unakuwa katika hali nzuri.

 

“Tutakuwewepo Mkwakwani kwa mzunguko ujao, juzi tu nimetoka huko kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa hasa hali ya uwanja, kulikuwepo na sehemu ambazo hazikuwa na nyasi hivyo tunajaribu kuhakikisha unakuwa katika hali nzuri” amesema Idrissa.

 

Ameongeza kuwa wameamua kuendelea na uwanja huo kutokana na hali nzuri ya mkoa wa Tanga ambayo imeweza kwenda sawa na mahitaji ya timu.

 

Azam FC katka mzunguko wa pili watacheza mechi sita tu wakiwa nyumbani huku mechi tano watacheza wakiwa ugenini, meza za nyumbani zitakuwa dhidi ya AFC ya Arusha, Police Tanzania, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Majimaji na Toto Africa wakati mechi za ugenini zitakuwa dhidi ya Simba SC, Yanga, Ruvu Shooting, Jkt Ruvu na African Lyon