Timu ya Azam FC inataraji kushiriki katika tamasha la AMKA kijana kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabigwa watetezi timu ya Simba SC, siku ya jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Azam FC watcheza mechi hiyo wakiwa na timu ya mchanganyiko kutoka Azam Academy na wale wa timu ya Azam FC kwani wachezaji nane wapo timu za taifa huku wengine wakiwa wmerejea makwao katika mapumziko.

 

Akithibitisha ushiriki wao Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa amesema timu itashiriki katika tamasha hilo ikiwa pia ni sehemu ya mwanzo ya maandalizi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu.

 

 

Azam FC kuanza mazoezi Nov 22

 

Kikosi cha Aza FC kinatarajia kuanza mazoezi ya matayarisho kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu siku ya Jumatatu, Novemba 22 jijini Dar es Salaam.

 

Timu itaanza mazoezi ikiwa na wachezaji waliobaki huku wakisubiri wengine ambao watajiunga na timu baada ya kutoka katika timu zao za taifa.

 

Wachezaji saba wa Azam FC wapo katika timu za Taifa za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes, waliopo wataanza mazoezi wakiwa chini ya kocha wao msaidizi Habib Kondo.

 

Katibu Mkuu wa Azam FC amesema timu inaanza mazoezi mapema ili kujiimarisha zaidi kwa ajili ya ligi hiyo kwani katika mechi ya kwanza waliweza kupoteza mechi tatu mfululizo.

 

Akizungumzia nafasi ya kocha mkuu, Idrissa amesema bado wapo katikamchakato kuhakikisha wanapata kocha bora na makini, hivyo ka kipindi hiki ambacho hawana kocha mkuu timu itaendelea kufundishwa na kocha msaidizi Kondo.