Kikosi kamili cha Azam FC leo' Jumapili' kitashuka katika uwanja wa Mkwakwani, kumaliza mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting.

 

Mechi ambayo Azam FC watacheza wakiwa na lengo la kusaka kubaki katika nafasi ya tatu ya ligi kuu, kwa kuondoka na ushindi katka mechi hiyo itakayochezwa mkoani Tanga.

 

Mohamed Sef 'King' Mratibu wa Azam FC amesema timu imefanya maandalizi ya kutosha kwajili ya mchezo, kwani wanaamini wanao uwezo wa kukaa katika nafasi ya tatu.

 

“Hapa tulipofikia hatuna wasiwasi, tumejiandaa vya kutosha kuweza kukaa katika nafasi hiyo, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kwa ajili ya kuanza msimu unaokuja tukiwa katika nafasi nzuri.” King

 

Amesema mechi na Ruvu Shooting itakuwa mechi muhimu sana kwao, mechi ambayo itawapa wakati mzuri wa kuanza maandalizi kwaajili ya mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuanza Januari 2011.

 

Azam FC ipo katika nafasi ya nne ikiwa na point 17, nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 19 ambayo imeshacheza mchezo wake wa mwisho, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Simba yenye pointi 24 ikifuatiwa na Yanga yenye point 22.

 

Mbali na mechi hiyo kutakuwa na mechi zingine Majimaji FC itacheza na Simba SC katika uwanja wa Majimaji, Songea, AFC itacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Police Tanzania itaikaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Jamuhuri Dodoma, huku Yanga watacheza na ndugu zao Toto African katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro