Timu ya Azam FC inatarajia kuondoka kesho 'Jumanne' mchana kuelekea mkoani Tanga kwa maandalizi ya mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom.

 

Azam FC itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Mkwakwani, mkoani humo siku ya Jumamosi.

 

Mratibu wa klabu hiyo Mohamed Seif 'King' amesema timu itakaa mkoani humo ikifanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mechi hiyo, mechi ambayo Azam FC inatakiwa kutoka na ushindi ili kumaliza mzunguko huo wakiwa katika nafasi ya tatu.

 

“Tunataraji kupata ushindi katika mechi hiyo, ili kumaliza vyema mzunguko huu, tutaondoka na wachezaji 24 kwa ajili ya mechi hiyo muhimu.

 

Azam FC itacheza mchezo huo ambao utakuwa mchezo wao wa kwanza kucheza bila ya kuwa na kocha wao Mkuu Itamar Amorim ambaye amesitisha mkataba wa kukinoa kikosi hicho.