Baada ya kutoka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na kufikisha ushindi wa mechi tatu wakiwa ugenini, timu ya Azam FC siku ya Jumapili yaani kesho jioni itaikaribisha Yanga katika uwanja wa Mkwakwani, mkoani Tanga.

 

Timu zote mbili zimesajili wachezaji kwa kubadilishana, Azam FC walimchukua MVP, Mrisho Ngassa kutoka Yanga, huku Yanga wakiwachukua Nsa Job na Yahya Tumbo.

 

Kocha wa Azam FC Itamar Amorin anatarajia kumtumia vema Ngassa kuleta ushindi, kama alivyofanya katika mechi zilizopita, akiwa anawafahamu vema mabeki na safu nzima ya Yanga kwani ameshacheza nao akiwa na klabu hiyo.

 

Ngassa ambaye anatarajiwa kufanya kama alivyofanya Ramadhani Chombo Redondo ambaye aliweza kuifunga Simba SC katika mechi ambayo Azam walifungwa 2-1.

 

Kwa upande wa Yanga wachezaji Nsa Job na Tumbo walicheza Azam kwa vipindi vya miaka miwili, nao kwa nafasi zao wanaweza kuzipatia ushindi timu yako kwa kutumia nafasi walizokuwanazo kwani wanafahamu uwezo wa wachezaji wa Azam.

 

Mechi hiyo ya tisa ya ligi kuu ya Vodacom, Azam FC watashuka dimbani wakiwa na pointi 13 huku Yanga wakiwa mbele kwa pointi saba, Azam FC wameshinda mchezo minne, wametoka sare mchezo mmoja na kupoteza michezo mitatu, wakat Yanga wameshinda michezo sita na kutoka sare michezo mwili huku wakiwa hawajapoteza hata mechi moja.

Hadi sasa yanga imeruhusu goli moja tu kwenye wavu wake huku kipa Mghana wake akiendelea kung'ara kwenye ligi