Azam FC siku ya Alhamis itashuka katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma kucheza na timu ya Majimaji FC katika mchezo wa saba wa ligi kuu ya Vodacom.

 

Mechi hiyo itakayokuwa ngumu kwa timu zote kwani zimepishana pointi moja huku Azam FC wakiwa na pointi 7 ikifuatiwa na Majimaji yenye pointi 6, ikiwa imeshinda michezo miwili tu na kupoteza michezo minne.

 

Azam FC iko wilayani Songea tangu siku ya Jumatatu itacheza mchezo huo ikiwa na lengo la kusaka pointi tatu muhimu ili kujiweka sawa katika ligi kuu.

 

Azam iliwasili ikiwa na timu kamili pamoja na wachezaji wote waliokuwa katika timu ya taifa, ikiwa na wachezaji zadi ya 20. wakitoka katika mechi wataweka kambi maalum kwa ajili ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar  itakayochezwa Jumanne ijayo Mkoani Morogoro huko Manungu