Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 'TFF' limemfungia miezi 6 mwamuzi Mathew Akram wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Azam FC na Simba, kwa kosa la kishindwa kutafsiri sheria za mchezo huo, ambao Simba walishinda 2-1.

Mchezo huo wa 7 ulichezwa katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, Septemba 11, mwamuzi huyo akishirikiana na mwamuzi msaidizi Frank Komba walishindwa kutafsiri sheria hizo kwa kutoa maamuzi yasiyosahihi yaliyoimiza timu ya Azam FC.

Waamuzi hao wamefungiwa kujihusisha na kazi hiyo kwa miezi sita kwa mujibu wa kanuni ya 26 (1a) ya sheria za mashindano za TFF. Maamuzi hayo yametolewa kutoka katika kikao cha kamati ya mashindano ya shirikisho hilo kilichoka siku ya jumatatu Septemba 27.

Kwa mujibu wa ushahidi wa kanda ya Video ambayo Azam FC iliwasilisha TFF pamoja na malalamiko yao, ilionekana dhahiri shahiri kuwa kosa la John Bocco lilikuwa la kugongana kwa bahati mbayana na Joseph Owino na kama mwamuzi angekuwa makini basi asingetoa kadi yoyote na kama angetoa kadi basi ingekuwa ya njano na siyo kadi nyekundu.

pia ushahidi huo ulionesha kuwa goli la pili la Simba lilikuwa ni la kuotea lakini kilichomkaanga zaidi mwamuzi huyo zilikuwa ni rafu ambazo Kevin Yondani alikuwa akimchezea Mrisho Ngasa mara kwa mara lakini mwamuzi alikuwa kimya.

Kuna  rafu ambazo Kevin alimfanyia Ngasa tena Ngasa akiwa mtu wa mwisho, wakati mwingine alitumia hata mikono kumzuia na sheria zinasema rafu kama zile ni kadi nyekundu moja kwa moja lakini mwamuzi alikuwa kimya na kuiumiza AzamFC

Mbali na waamuzi hao pia waamuzi Ronald Swai na msaidizi wake namba mbili Samuel Mpenzu watatumikia kifungo hicho kwa kosa la kutotafsiri vyema sheria za mpira na kusababisha Yanga kufunga goli la kwanza katika mechi ya 26 kati ya Yanga na Kagera Sugar, na kamishna wa mchezo huo amefungiwa miezi 12 kwa kutoandika taarifa sahihi.