Azam FC kesho Jumatano itaingia uwanjani kusaka pointi tatu dhidi ya maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Azam FC ikiwa na jumla ya pointi 6 sasa itashuka dimbani kwa matumaini zaidi baada ya kuizamisha African Lyon 2-1 katika mchezo wa 5 uliochezwa katika uwanja huo.

Wakiwa nyumbani, Azam FC wanamatumaini ya kushinda mchezo huo “Tumeamsha morali na kupata matumaini zaidi baada ya kushinda mechi dhidi ya Lyon ambayo yatatusaidia kuweza kushinda katika mechi yetu ya jumatano” amesema nahodha mkuu wa kikosi hicho Salum Swed 'Kussi'.

Swedi amesema wachezaji wamepata hamasa ambayo waliipoteza kwa kufungwa mechi tatu mfululizo, hivyo kwa mechi zijazo ushindi utapatikana kwani wanafanya mazoezi ya nguvu kukabiliana na timu pinzani.

Azam FC imeshinda mechi mbili kati ya tano, ina jumla ya magoli ya kufunga matano na kufungwa matano, inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi inayoongozwa na Yanga yenye pointi 16 na Simba yenye pointi 12.

Habari imeandikwa na SpaceRose Joseph aliyeko Tanga