Ikiwa katika maandalizi ya mechi dhidi ya JKT Ruvu, Azam FC leo imeifunga 2-1 timu ya Coastal Union katika mchezo wa kirafiki iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.Azam wakicheza kikosi cha pili, kipindi cha kwanza walitoka bila kufungana.

Waliporejea kipindi cha pili Azam FC walianza mashambulizi na dakika ya 47 Peter Ssenyonjo alifunga goli la kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Jamal Mnyate.  

Dakika tatu baadae, Mnyate aliandika goli la pili baada ya kuwatoka  mabeki wa Coastal katikati ya uwanja. Mnyate  akiwa nyota wa mchezo amecheza katika kiwango cha hali ya juu akishirikiana vyema na mchezaji wa kimataifa Ssenyenjo ambaye wamecheza muda wote wa dk 90.Pia kazi nzuri ya mabeki na viungo vijana kama Tumba Swed, Ibrahim Jeba, Samir Nuhu, Himid Mao na Faraj Hussein iliweza kutoa ushindani mkubwa kwa Coastal Union walionekana kukatika mara kwa mara.Goli pekee la Coastal lilifungwa na Bariki Dimoso