Wakazi wa jiji hilo wamesema ingawa timu hiyo haijafanyiwa haki katika mechi iliyopita wataendelea kuishangia muda wote kwani kuuchagua uwanja wa Mkwakwani ni heshima kwa mkoa huo.

 

Tanga imeweza kushuhudia mechi za ligi kuu zaidi ya miaka mitano iliyopita wakati ikiwakilishwa na klabu kongwe ya mji huu Coastal Union ambayo tangu iliposhuka daraja hakukuwa na mechi yoyote ya ligi kuu iliyochezwa jijini humo.

 

Aliyekuwa katibu mkuu wa Coastal Union Salim Bawazir amesema Azam FC imetoa fursa nyingine kwa wakazi wa Tanga kwa kuuchagua kama uwanja wao wa nyumbani, hiyo italeta changamoto zaidi kwa mkoa.

 

“Azam FC wamerejesha faraja kwa wakazi wa Tanga, wametupa nafasi ya kushuhudia mechi za ligi kuu hivyo ni wakati wetu kuendelea kuipa 'support' timu hiyo, kwa kipindi chote watakachokuwa hapa jijinikwetu.” amesema Bawazir.

 

Bawazir amewataka viongozi wa Azam FC kuondoa wasiwasi kwani uwanja ni wao hivyo wajisikie wapo nyumbani na kutoa ushirikiano mzuri kwa wakazi na viongozi kama walivyofanya katika meci yao ya kwanza dhidi ya Simba.