Kikosi kamili cha Azam FC kimeingia jijini Tanga mchana wa leo kikitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza mechi yake ya pili ya ligi kuu dhidi ya Simba SC, katika uwanja wa Mkwakwani.

 

Azam FC inayotumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani, lakini leo wanafanya mazoezi ya jioni katika uwanja wa Popatlal Sec School uliopo jijini humo.

 

“Tumefika salama, tunamshukuru Mungu, timu inaanza mazoezi leo jioni katika uwanja huo kwa kuwa uwanja wa Mkwakwani unatumika kwa shughuli nyingine ya mkoa.” amesema Mratibu wa Azam FC Mohamed Seif 'King'.

 

Azam FC itakuwa Tanga kwa siku tatu kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya safari ya kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mechi ya tatu itakayochezwa siku ya Jumatano dhidi ya Kagera Sugar.