Siku moja baada ya Taifa Stars kutoka sare ya 1-1 na Algeria katika mechi za kufuzu kucheza fainali za kombe la Mataifa ya Africa, Kocha wa Azam FC, Itamar Amorim amesifu kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wote wa timu ya Taifa hasa wale wanaochezea timu yake.

 

Katika mechi hiyo Azam FC iliwakilishwa vyema na wachezaji watano ambao kwa nafasi zao wameweza kusaidia timu hiyo kupata matokeo hayo muhimu kwa timu ya Taifa.

 

“nimeangalia mechi yote, wachezaji wangu wamejitahidi kucheza vizuri, ilikuwa mechi ngumu sana kwa timu yetu kupata sare hiyo kwani Algeria ni timu nzuri Africa na imetoka katika fainali za kombe la dunia siku chache zilizopita” amesema Itamar.

 

Itamar ameongeza kuwa mafanikio katika mechi ya jana ni juhudi pia za wachezaji wote wa Stars, Stars imeanza vizuri kutafuta nafasi hiyo ikiongeza bidii zaidi itaweza kucheza fainali hizo.

 

Goli la Abdi Kassim lilikuwa zuri sana lakini Aggrey Morris na Nadir Haroub Canavaro walicheza vizuri sana jana.

 

Wachezaji wa Azam FC walicheza ni Mrisho Ngassa, Aggrey Moris, Erasto Nyoni, Jabir Aziz na Seleman Kassim 'Selembe', mbali na wachezaji Stars ya jana iliundwa na Shaaban Kado, Stephano Mwasika, Nizar Khalfan, Nadir Haroub, Henry Joseph, Idrissa Rajab, DannyMrwanda, Shadrack Nsajigwa.