Kikosi cha wachezaji 22 wa Azam FC wamewasili mkoani Arusha tayari kwa kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya AFC katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku ya Jumamosi.

 

Azam FC wameondoka jijini Dar es Salaam alfajiri ya saa 11, wamewasili mkoani humu saa 7 mchana, Mratibu wa klabu hiyo Mohamed King amesema timu imefika ikiwa salama.

 

“tunashukuru tumefika salama, timu imefanya mazoezi ya jioni katika uwanja wa General tyre na itaendelea na program ya mazoezi kama kawaida.” amesema King

 

Mratibu ameongeza kuwa timu itafanya mazoezi kesho asubuhi, jioni itaenda kuangalia mechi ya AFC itakayocheza dhidi ya timu ya JKT ya mkoni humo.

 

King amesema katika msafara huo wameacha wachezaji Ibrahim Mwaipopo anayesumbuliwa na nyama za paja, Ally Manzi mwenye matatizo ya kifamilia, wachezaji waliopo timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes waliopo Eritrea na golikipa Daudi Mwasongwa aliye safiri leo kuelekea Eritrea baada ya golikipa Wandwi Willium kuvunjika mkono.

 

 

Kikosi kilichopo Arusha ni Jackson Chove, Jabir Aziz ,Ramadhan Chombo 'Redondo' , Mrisho Ngassa, Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' Patrick Mutesa Mafisango na Peter Senyonjo. John Bocco, Erasto Nyoni,

 

Wengine ni Jamal Mnyate, Vladmir Niyonkuru, Philip Alando, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Aggrey Morice, Salum Swed, Ibrahim Shikanda, Seleman Kasim 'Selembe' na  Ali Mkuba na Samih Nuhu.

 

 

 

Wandwi avunjika mkono Eritrea

 

Golikipa wa timu ya Azam Academy, Wandwi Willium amevunjika mguu akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes kilichopo katika mashindano ya kombe la Challenge kwa vijana.

 

Nafasi yake inachukuliwa na kipa mwingine wa Azam FC Daudi Mwasongwa aliyeondoka leo kuelekea nchini humo.