Azam FC leo imepoteza mechi yake ya kirafiki kwa kuruhusu kufungwa 3-2 na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo Azam FC ilionesha upinzani mkali katika kipindi cha kwanza timu zote zilitoshana nguvu kwani hadi kufikia mapumziko kulikuwa hakuna timu iliyoweza kuona goli la mwenzake.

Mchezaji wa Azam FC, Kally Ongala aliweza kukonga nyoyo za mashabiki wa Azam kwa kucheza katika kiwango cha juu na kuonyesha uwezo wake.

Kipindi cha pili timu zote ziifanya mabadiliko kwani waliweza kuonyesha kiwango cha juu, dakika ya 48 Mtibwa Sugar walipata goli la kwanza kupitia kwa mchezaji Yona Ndabila aliyeachia shuti lililomuacha kipa Vladimir Niyonkuru na kutinga wavuni.

Dakika nane baadaye Azam FC wanapata goli la kusawazisha kwa njia ya penalt iliyopingwa na mchezaji Patrick Mafisango, baada ya Mrisho Ngassa kuangushwa katika eneo la hatari.

 

Dakika ya 58 Azam FC walipata goli la pili baada ya mchezaji John Bocco kutoa pass kwa mchezaji Seleman Kassim na kuandika goli hilo.

Mtibwa Sugar walianza mashambulizi ya kutafuta ushindi kwani dakika ya 65 Ndabila aliandika goli la pili kwa mpira wa kichwa iliyomuacha kipa namba mbili wa Azam FC Jackson Chove.

Wakiwa na nia ya kutafuta ushindi Mtibwa Sugar walitoa mashambulizi mbalimbali, huku Azam FC wakifanya mabadiliko kubadilisha matokeo hayo lakini haikuwezekana kwani dakika ya 80 Mtibwa walipata goli la ushindi kupitia kwa mchezaji wake Omary Matuta aliyepokea mpira wa kona uliopigwa na mchezaji Saidi Mkopi.

Mtibwa Sugar Shaaban Kado, Juma Abdul, Yusuph Mguya, Faustin Lukoo/Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Lameck Dayson/Vicent Barnabas, Boban Zilintusa, Thomas Moris, Yona Ndabila, Salum Machaku.

 

Vladmir Niyonkuru/Jackson Chove, Obrahim Shikanda, Agrey Morris, Patrick Mafisango, Salum swed, Jabir Aziz, Ramadhan Chombo, Seleman Kassim/ Jamal Mnyate, John Bocco, Mrisho Ngassa/ Philip Alando, Kally Ongala/ Jafary Hussein,   

 

 

Kocha mkuu wa Azam FC Itamar Amorim amesema matokeo ya mchezo huo ni sehemu ya mpira, hivyo anayachukulia kama sehemu ya maandalizi kwani bado wiki moja kuanza kwa ligi kuu.

“Tumepoteza mechi ambayo ni mechi yetu ya kwanza kupoteza katika majaribio, nimeona baadhi ya makosa hivyo hayatajirudia tena katika mechi zetu za ligi kuu.” Anasema Itamar.

 

Naye kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar Meck Mexime amesema matokeo ya mechi ya leo ni sehemu yao ya marekebisho kwa timu kwani ligi karibu inaanza hivyo matayarisho zaidi yanahitajika.

 

“Tumeshinda mchezo wa leo lakini kuna mapungufu yameonekani hivyo tutayatafanyia kazi ili kujiweka sawa na mechi zetu za ligi kuu.” Amesema Mexime.