GOLI lililofungwa na Peter Ssenyonjo katika kipindi cha pili lilitosha kuipa ushindi timu ya Azam FC ambayo ilikuwepo kisiwani hapa kwa takribani wiki mbili ikijiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League

Azam FC ambayo jana iliwakosa wachezaji wake takribani kumi kutokana na kuwa na timu za taifa za Ngorongoro Heroes na Taifa Stars ilicheza mchezo mzuri na wa kuvutia sana hapo jana.

Hivi ninapoandika taarifa hizi, timu ya Azam FC ipo kwenye Boti ikirejea jijini Dar es Salaam ambapo inatarajia kucheza michezo mingine ya kirafiki jijini Dar es Salaam wiki ijayo. 

Kuna taarifa kuwa, chama cha soka cha Zanzibar ZFA kimeialika tena timu ya soka ya Azam FC kisiwani Zanzibar kucheza na timu ya Vijana Karume Boys baadaye wiki ijayo