Zikicheza soka la kirafiki na mazoezi, timu za Azam FC na Simba SC zilitoka ya bila kufungana katika mchezo mzuri na wa kuvutia uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar

Simba ilianza ilichezesha timu mbili tofauti kila kipindi huku Azam FC ikiwaweka benchi wachezaji wake mahiri kama Ramadhani Chombo Redondo, Ibrahim Mwaipopo, Patrick Mafisango, Mrisho Ngasa na Jackson Chove.

Haukuwa mchezo wa kukamiana, tumecheza mchezo wa kindugu na kirafiki tukiziandaa timu zetu na ligi kuu ya Vodacom alisema Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu.

Katika mchezo wa jana mchezaji Jabir Aziz alionesha soka la hali ya juu sana kama ilivyokuwa kwa Kalimangonga Ongala na Mohammed Binslum ambao waling'ara sana uwanjani hapo jana.

Azam FC iliwachezesha Vladmir Niyonkuru ambaye baadaye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Daudi Mwaisongwe, Ibrahim Shikanda alicheza kama beki wa kulia, Mau Bofu alicheza kushoto na baadaye alitoka na kumpisha Malika Phili Mdeule, Aggrey Morris alitoka na kumpisha Salum Swedi, Erasto Nyoni alicheza kama sentahaf, Alli Mkumba alicheza kiungo wa nyuma, na Jabir Aziz alicheza kiungo cha mbele na baadaye alimpisha kinda Faraj Husein, Selemani Kassim alicheza kulia na kushoto alicheza Mohammed Binslum na baadaye alitoka na kumpisha Jamal Mnyate, Kaly Ongala alicheza na John Bocco kama washambuliaji na baadaye walitoka na kuwapisha  Peter Ssenyonjo na Philip Alando