Ili kujiweka sawa zaidi kwa ajili ya ligi kuu, timu ya Azam FC siku ya Jumamosi usiku itacheza mechi ya kirafiki na Simba SC katika uwanja wa Amani Karume mjini Zanzibar.

Azam FC itacheza mechi hiyo ambayo itakuwa ya pili wakiwa visiwani huko huku mechi ya kwanza inatarajiwa kufanyika kesho dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja huohuo.

 

Mratibu wa Azam FC, Mohamed King amesema timu iko katika hali nzuri kucheza mechi zote za kirafiki kwani inafanya mazoezi ya hali ya juu kwa maandalizi ya ligi kuu.

 

Timu inafanya mazoezi kwa siku mara mbili, hivyo mechi hizo za kirafiki ni sehemu ya kujipima ili kujiweka sawa kwa ajiliya ligi kuu itakayoanza hivi karibuni” amesema King.

 

Akizungumzia kuhusu hali ya mchezaji Mrisho Ngassa, King amesema hali ni nzuri na anaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine.

 
Hakuna uhakika na uwepo wa mechi na Express FC
Wakati huohuo, ile mechi iliyotangazwa hapo awali kati ya Azam FC na Express FC ya Uganda huenda isiwepo kufuatia kuibuka kwa taarifa zinazochanganya kati ya waandaaji na klabu ya Yanga ambao pia walipaswa kucheza mechi hiyo.
 
Vyovyote itakavyokuwa Azam FC ipo tayari kucheza mechi hiyo kama FC Express itawasili