TIMU ya Express ya Uganda inatarajiwa kutua nchini kucheza mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya Yanga na Azam FC zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Tanzania Daima le linaripoti kuwa, Kwa mujibu wa msemaji wa Kampuni ya LZ Enterprises ya jijini Dar es Salaam, George Wakuganda, Waganda hao wataanza kukwaana na Yanga hapo Jumamosi.

Alisema baada ya mechi hiyo ambayo Yanga itaitumia kupima vifaa vyake vipya, Agosti mosi, Yanga itacheza na Azam FC.

Mfulizo wa mechi hizo, zitaendelea tena Agosti 2 ambapo Express itakwaana na Azam FC ambayo nayo itakuwa ikipima nyota wake wapya akiwemo Mrisho Ngassa aliyesajiliwa kutoka Yanga.

Ngassa, kati ya wachezaji walio kwenye kiwango cha juu kiuchezaji, ametua Azam FC kwa kitita cha shilingi mil. 58.