Timu ya Azam FC leo Jumatatu ya tarehe 26/July itakwenza visiwani Zanzibar kuweka kambi ya siku 13 ikiwa ni sehemu ya program ya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu ijayo inayoatarajiwa kuanza August 21.

Kikosi kamili cha timu hiyo kitaondoka jijini na boti za kampuni ya Azam Marine saa 6:30 mchana kuelekea visiwani humo ambako watacheza mechi tatu za kirafiki kabla ya kurejea jijini kuendelea na mazoezi.

 

“Wakiwa visiwani Zanzibar watacheza mechi tatu za kirafiki, watacheza na timu ya Zanzibar Ocean view, KMKM na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, mechi ambazo zitasaidia kuiweka timu katika hari nzuri kupambana katika ligi.” amesema Katibu mkuu wa klabu, Nassir Idrissa.

 

Amesema timu itarejea tarehe tarehe 08/08 kuendelea na maandalizi mengine muhimu katika kipindi cha wiki mbili tu kabla ya kufunga sfari kuifuata AFC ya Arusha katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ikayochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid.

 

Wachezaji Azam FC watibiwa meno

 

Wachezaji wa timu ya Azam FC leo wamefanyiwa matibabu ya meno katika hospitali ya Manispaa ya Kinondoni, Mwananyamala kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya ligi kuu ya 2010/2011.

 

Wakiongozwa na viongozi wa klabu hiyo wachezaji wote walioenda waligundulika na tatizo la meno, na kupatiwa huduma ya kusafiswa papo hapo

 

Katibu Nassor Idrissa amesema baada ya kugundua tatizo hilo wachezaji wote walianza kupatiwa huduma ya kusafishwa meno yao na waliokuwa na matatizo mengine walipewa matibabu hospitalini hapo.

 

“Tumewapeleka wote hospital, wakagundulika na matatizo katika meno, ikabidi tuwasiliane na madaktari watano wataalam wa magonjwa ya meno na kuanza kuwatibu, tumefanya hivyo kuepuka kuwa na wachezaji wangonjwa pindi ligi itakapoanza” alisema Idrissa.

 

Idrissa amesema viongozi wote wa benchi la ufundi walipimwa afya zao isipokuwa kocha mkuu Itamar Amorin, amewataja waliopatiwa huduma hiyo kuwa ni meneja wa timu, Ibrahim Jeshi, kit manager Hamis Mbembe, makocha Hamis Jafary, Habib Kondo, Mohamed King na Iddi Aboubakari.