Baada ya kutoa sare na Ngorongoro Heroes, Azam FC leo imepata ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Ruvu Mkoani Pwani.

 

Azam FC ilianza kupata goli la kwanza dakika ya  15 ya mchezo lililofungwa na mchezaji John Bocco baada ya kuunganisha krosi ya Faraji Hussein.

 

Goli hilo lilidumu kwa dakika 20, baada ya beki wa kutumainiwa wa Azam FC, Aggrey Morice kuandika goli la pili kwa mpira wa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo  uliyopigwa kiufundi na Ibrahim Mwaipopo.

JKT walipata penati katika dakika za mwisho kipindi cha kwanza lakini golikipa mpya wa Azam Jackson Chove aliokoa

 

Matokeo hayo yalizipeleka timu zote mbili mapumziko, huku Azam FC ikiongoza kwa 2-0.

 

Kipindi cha pili tiu Azam FC ilifanya mabadiliko kuimarisha ngome yake kwa kumtoa Erasto Nyoni na Seleman Kassim ‘Selembe’ na nafasi zao zikachukuliwa na Salum Swed na Jamal Mnyate.

 

Dakika ya 51 Ruvu Shooting walipata goli kupitia kwa mchezaji Salum Kimai baada ya kuachia shuti lililotinga wavuni na kumuacha kipa wa Azam FC, Jackson Chove akishangaa.

 

Goli hilo lilileta mabadiliko ya mchezo kwani timu zote zilicheza kwa kukamiana huku Ruvu Shooting wakitaka ushindi katika mechi yao ya nyumbani, na Azam wakiitaji kulinda lango wasipoteze mechi ya leo.

 

Katika mechi hiyo ya kirafiki, golikipa Jackson Chove alipewa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga mchezaji Paul Ndauka na mchezaji wa Ruvu Shooting Gido Chawala alipewa kadi nyekundu baada ya kumsukuma Chove baada ya kumfanyia madhambi Ndauka.

 

Kocha wa Azam FC,Itamar Amorin amesema kikosi chake kimebadilikana kuimarika kuliko walipokuwa wakicheza mechi yao ya kwanza.

 

“Timu imecheza vizuri, kuna mabadiliko makubwa hasa upande wa pasi, ball position na ball control ukilinganisha na mechi iliyopita, kwani wameimarika zaidi.” Alisema Itamar.

 

Ameongeza amerekebisha makosa yaliyotokea katika mechi dhidi ya Ngorongoro, na kuifanya timu hiyo kuwa katika hali nzuri zaidi.

 

Akizungumzia uwanja wa Ruvu, Itamar alisema ni uwanja mzuri, una nyasi nzuri lakini zimezidi sana na hazifai kwa kuchezea mpira kwani mpira unakwama mara na kupoteza pasi za wachezaji.

 

 

Azam FC, Jackson Chove/David Mwasongwe, Ibrahim Shikanda/Malika Ndeule, Mau Bofu, Agrey Morice, Erasto Nyoni/Jamal Mnyate, Ibrahim Mwaipopo, Faraji Hussein/Ally Mkuba, Ramadhani Chombo ‘Ridondo’, John Bocco/Ally Manzi, Mrisho Ngassa/Cosmas Lewis, Seleman Kassim/ Jamal Mnyate.

 

 

Yonatus Mbalimo, Mangasin Mbomus, Peter Moses, George Akitenda, George Osey, Owen Mikumba, Godo Chawala, Faraji Makumbo, Martin Lupati, Salum Chimai, Revocatus Maliwa.