Timu ya Azam FC imeanza kwa kutoka sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes katika mechi ya majaribio iliyochezwa Uwanja wa Uhuru.

Azam FC iliyoingia kambini wiki iliyopita leo imecheza mchezo wake wa kwanza wa majaribio ikiwa nawachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu unaotarajiwa kuanza Agost 21mwaka huu.

Wakiwa bado hawajazoeana vizuri Azam FC ilitoshana nguvu na kikosi cha Ngorongoro Heroeskinachojiandaa kwa ajili ya kucheza mchezo wa mwisho wa kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana dhidi ya Ivory Coast wiki ijayo.
 
Mchezo huo ulianza majira ya saa moja na nusu asubuhi, Azam walitoa mashambulizi mara kwa maralakini hayakuweza kuzaa matunda kwani Ngorongoro Heroes walikuwa na ulinzi imara uliowazuiawachezaji nyota kama Ramadhan Chombo ' Ridondo', Jabir Aziz na John Bocco.
 
Wakitumia mpira aina ya Jabulani, dakika ya 14 Ngassa alikosa goli baada ya kupiga shuti lililotokanje, dakika ya 30 alishindwa kuunganisha krosi ya Bocco na mpira ukatoka nje, dakika ya 29 Boccoalishindwa kutuliza mpira na kupiga mpira uliotoka nje.
 
Upande wa Ngorongoro walicheza kwa kasi ya ajabu, walishambulia mara kwa mara lakinihawakuweza kufunga, wachezaji Mbwana Samata, Issa Rashid na Rajab Isihaka walitumia vibayanafasi za wazi.
 
Kipindi cha pili Azam FC waliiga mfumo wa Ivory Coast kwa kubadili timu nzima lakini nayo haikuwezakutikisa nyavu za Ngorongoro Heroes.
 
Nao Ngorongoro Heroes kipindi cha pili walifanya mabadiliko machache kwa kuwaingiza JeromeLambele, Ibrahim Jeba na Yusuph Soka lakini hawakuweza kubadilisha matokeo hayo.
 
Azam FC, Vladmir Niyonkuru/Jackson Chove, Ibrahim Shikanda/Salum Swed, Mau Ally/ALLY Mkuba,Agrey Morice/Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni/Faraji Hussein, Ibrahim Mwaipopo/Cosmas Lewis,Ramadhan Chombo/Malika Ndeule, Jabir Aziz/Ally Nuhu, John Bocco/Ally Manzi, Mrisho Ngassa/PhilipAlando, Seleman Kassim/Jamal Mnyate.
 
Saleh Kabali, Salum Telela, Aman Kiata, Tumba Swed, Himid Mao, Omega Seme, Aboubakar Salum,Rajab Isihaka, Issa Rashid, Mbwana Samata, Abou Ubwa.
.
Alando avaa namba 15
 
Baada ya namba yake kuchukuliwa na mchezaji mwenye gharama kubwa kuliko wote Tanzania 'MVP'Mrisho Ngassa, mchezaji mkongwe Philip Alando sasa anavaa jezi yenye namba 15.
 
Alando tangu alipojiunga na timu ya Azam FC amekuwa akiivaa jezi hiyo kabla ya kuchukuliwa namchezaji huyo aliyetokea Klabu kongwe ya Yanga.
 
Ngassa amekuwa akiitumia jezi hiyo tangu alipokuwa Yanga na mechi kadhaa akiwa na timu ya taifaambapo sas anavaa jezi namba nane akiwa na timu ya taifa.
 
 
*******
Jezi namba,
22 Vladmir Niyonkuru, 21 Ibrahim Shikanda, 26 Mau Ally, 13 Aggrey Morice, 6 Erasto Nyoni, 4 IbrahimMwaipopo, 30 Ramadhani Chombo, 25 Jabir Aziz, 19 John Bocco, 16 Mrisho Ngassa, 7 SelemanKassim 'Selembe', 12 Jackson Chove, 2 Salum Swed, 29 Ally Mkuba Sisoko, 5 LucksonKakolaki, 27Faraji Hussein, 18 Cosmas Lewis, 20 Malika Ndeule, 11 Samih Nuhu, 9 Ally Manzi, 15 Philip Alando, 17 Jamal Mnyate.
 
 
 
 
Rodrigo: Azam wapo vizuri
 
Baada ya kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Azam FC, kocha mkuu wa Ngorongoro Heroes Rodrigo Stockler amesema wachezaji wa Azam wamefanya vizuri kulingana na muda ambaowameanza mazoezi.
 
“Azam ya sasa inawachezaji wengi walio na uzoefu hasa wale wanaocheza katika timu ya taifa, wanauwezo mzuri na kwa kipindi cha muda mfupi wameweza kucheza kitimu, wanaelewa japo kunamapungufu kidogo lakini watafanya vizuri zaidi.” amesema Rodrigo.
 
Amesema Itamar Amorin amelenga zaidi kuchukua ubingwa wa ligi kuu, na kutokana na mazoezi namafunzo anayowapa wachezaji wake atafikia malengo yake.
 
Akizungumzia uwezo wa wachezaji waliojiunga na timu hiyo, Rogrigo amesema wameonesha mchezomzuri, wamecheza vizuri lakini walikuwa wanakabiliwa na kutokuzoeana tatizo ambalo huwa ni lamuda mfupi.
 
Ameongeza kuwa kikosi cha Azam FC kilichocheza leo kimewakosa wachezaji wake waliopo katikatimu ya Ngorongoro, wakiungana pamoja watakuwa na timunzuri na imara.