ikiwa imesalia siku moja kufikia mwisho wa usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu utakaoanza August mwaka huu, uongozi wa Azam FC umetangaza kukamisha usajili wake na kuanza kwa maandalizi kwa ajili ya ligi hiyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed amesema usajili wa mwaka huu wameacha wachezaji kumi waliokuwepo msimu ulipita na kubakisha wachezaji 14, huku wakisajili wachezaji wapya nane na kupandisha jumla ya wachezaji sita kutoka katika timu ya vijana 'Azam Academy'. “Katika usajili wetu tumesajili wachezaji watatu kutoka nje ya Tanzania na watano kutoka katika vilabu vya hapa nchini, tumezingatia taratibu za TFF kwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano, ni matumaini yetu wachezaji wetu watafanya vizuri” alisema Mohamed. Mohamed aliongeza kuwa Azam itakuwa na jumla ya wachezaji watano wa kigeni baada ya kuongeza wachezaji watatu ambao wataungana na wengine wawili walipo katika timu hiyo.

 

Uongozi umewataja wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo kuwa ni Mohamed Binslum (Huru) Jackson Chove(JKT Ruvu), Jabir Aziz na Ramadhan Chombo 'Redondo' (Simba), Mrisho Ngassa (Yanga), Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' (GIF-Sweeden), Patrick Mutesa Mafisango (APR- Rwanda) na Peter Senyonjo (Polisi-Uganda.)

 

Wachezaji waliobaki ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jamal Mnyate, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Vladmir Niyonkuru, Philip Alando, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Aggrey Morice, Salum Swed, Ibrahim Shikanda, Ally Manzi, Seleman Kasim 'Selembe' na Ibrahim Mwaipopo.

 

Makamu Mwenyekiti aliongeza kuwa timu hiyo haikuwaacha mbali wachezaji wao wa timu ya vijana 'Azam Academy', imepandisha wachezaji sita ambao ni Sino Augustino, Himid Mao, Mau Ali, Tumba Swed, Ali Mkuba na Samih Nuhu. 

Mohamed aliwataja wachezaji walioachwa kuwa ni Chrispin Odula, Habib Mhina, Maridad Haule, Nsa Job, Said Swed, Salum Machaku, Yahya Tumbo, Ben Kalama, Shaaban Kisiga na Dan Wagaluka.