Baada ya kuwa mapumziko kwa takriban miezi miwili timu ya Azam FC leo Jumatatu imeanza rasmi mazoezi katika uwanja wa Uhuru ikiwa ni matayarisho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya 2010/11 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi ujao. Timu ya Azam FC leo ikiwa na wachezaji 23 walioripoti katika mazoezi imefanya mazoezi mbalimbali ya viungo katika program ya kufanya mzoezi kwa siku mara mbili asubuhi na jioni. Kocha Mkuu wa timu hiyo, Itamar Amorin amesema timu ilianza kwa mazoezi mepesi ya kujenga viungo na sasa wapo katika sehemu ya mwisho ya mazoezi hayo na kuanza mazoezi ya kucheza na mpira. “Tulianza mazoezi ya kujenga misuli wiki iliyopita na sasa tunamalizia ili tuanze mazoezi ya kucheza na mpira, mazoezi ambayo yatasaidia kuiweka timu sawa kwa ajili ya ligi kuu inayokuja.” alisema Utamar. Aliongeza kuwa hadi leo wachezaji 23 tu ndio walioanza mazoezi huku wachzaji wanne wakiwa bado hawajawasili, wachezaji hao ambao watatu wa kigeni na mkongwe Philip Alando anayetarajiwa kuwasili siku ya jumanne akitokea Mwanza.