BOCCO anaaminika kuwa mshambuliaji mrefu zaidi kwenye ligi kuu akiwa na mita 1.9  na uzito wa kila 76, ana umri wa miaka 21 tuu lakini kwa sasa hakuna ubishi kuwa huyu ndiye mshambuliaji bora kwa sasa ligi kuu ya Vodacom.

Raundi ya kwanza haikuwa nzuri kwake, baada ya kufunga magoli mawili safi kwenye mechi ya kwanza dhidi ya AFC, alipata balaa la kutolewa nje kwa kadi nyekundu kiuonevu kwenye mechi dhidi ya Simba na baada ya hapo hakuweza kufunga tena hadi raundi ya kwanza ilipomalizika.

John Bocco kijana mpole anayependa sana kufanya mazoezi binafsi pila ailiathirika na mfumo wa upangaji timu uliokuwa ukitumika kwenye klabu ya Azam FC ambapo alikuwa akitakiwa kucheza na Mrisho ngasa mchezaji mwenye kasi zaidi yake lakini timu ilikuwa ikikosa mpishi wa magoli na mipira ya krosi ambayo yeye ni mtaalamu wa kutumia mipira ya krosi.

Bocco mwenye uwezo wa kupiga faulo, anayetumia miguu yote na ambaye ana uhodari wa kupiga vichwa hivi sasa anafurahia maisha yake kama mchezaji akifunga magoli mawili katika kila mchezo mechi tatu mfululizo zilizopita.

Mchezaji ambaye watoto wadogo walimbatiza jina la Adebayor ambaye mjumbe wa kamati ya utendaji TFF Msafiri Mgoi anaamini kuwa ana kipaji cha hali ya juu kwani watoto hawana upendeleo wala hawakosea na kama wamemfananisha na Adebayor basi ana uwezo mkubwa amerejeshwa tena kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Msimu uliopita alifunga magoli saba katika mechi sita za awali akifunga goli kila mchezo michezo sita mfululizo, safari hii amerudia tena kwa kufunga magoli sita mechi tatu mfululizo akianza kwa kuwafunga Simba, kasha AFC na jana kuwafunga Toto Africa akifunga magoli mawili kila mechi.

Kwa sasa Bocco amefikisha magoli nane, Ngasa ambaye ni mchezaji ghali zaidi nchini anaongoza akiwa na magoli 10 na Gaudensi Mwaikimba wa Kagera Sugar akiwa na magoli tisa akishika nafasi ya pili.

Mtandao wa Azam FC www.azamfc.co.tz unaamini kuwa msimu huu Bocco au MVP wa Tanzania Mrisho Ngasa mmojawao ataibuka mfungaji bora VPL, au wote kwa pamoja , Viva John Raphael Bocco, Viva Mrisho Ngasa