UONGOZI wa klabu ya Azam umebaini mchezo mchafu uliotakwa kuchezwa na viongozi wa Yanga wa kutaka mchezaji Mrisho Halfan Ngassa kufungiwa kwa kusaini mikataba miwili katika klabu tofauti.

Mchezaji huyo amesajiliwa na Azam kwa shilingi 58milioni akitokea Yanga ambako ameichezea kwa kipindi cha miaka minne na kuwa mchezaji pekee aliyevunja rekodi kwa kusajiliwa kwa dau kubwa hapa nchini na kuvunja rekodi ya Juma Kaseja aliyesajiliwa Yanga kwa 38m msimu wa 2007/2008.

Gazeti la mwananchi toleo la leo limeandika, Habari za uhakika ambazo Mwananchi ilizipata ni kwamba viongozi wa Yanga walikuwa wakifanya mazungumzo na mchezaji huyo ili aweze kurudi Yanga na kusaini mkataba mwingine huku tayari akiwa ameshajifunga Azam kwa kusajili mkataba.

Imesemekana nia na madhumuni ya viongozi hao ni kutaka mchezaji huyo afungiwe na TFF kwa kusaini mkataba sehemu mbili ili asiweze kuichezea Azam msimu ujao, lakini mchezaji huyo aliwakatalia viongozi hao na kudai kuwa hawezi kurudi tena Yanga.

” Yanga walitaka kucheza mchezo mchafu kwa kumsainisha mchezaji huyo na kuwarudishia fedha Azam kitu ambacho Azam na Ngassa walikiona mapema na kuwakatalia,” alisema mtoa Habari.

Alisema kitu kilichowafanya Yanga kuanza kumsaka mchezaji huyo ni kanuni mpya ya TFF, iliyotaka klabu zote kusajili wachezaji watano tu wa kigeni kitu ambacho wanaona bado kitakuwa sio msaada kwao, ambapo ni bora wamrudishe mchezaji huyo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa bado klabu hiyo inafanya mazungumo na baadhi ya wachezaji akiwemo Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye mpaka jana alikuwa bado hajafanikiwa kusaini mkataba katika klabu hiyo.