Mchezaji Ramadhani Chombo ‘Ridondo’ amekuwa mchezaji wa tano kusaini kuichezea timu ya Azam FC akitokea klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.

Chombo amesajiliwa na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kumaliza mkataba wake mapema mwezi huu na klabu ya Simba.

Mchezaji huyo mwenye uwezo wa pekee ataungana na wachezaji wengine wanne waliosajiliwa kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo katika msimu unaokuja.

Chombo anaungana na Jabir Aziz, Mrisho Ngassa na Peter Senyonjo waliosajiliwa kwa miaka miwili kila mmoja na Jackson Chove aliyejunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.