Mshambuliaji Mrisho Ngassa aliyesaini kuichezea timu ya Azam FC kwa misimu mitatu ijayo ameapa kuisaidia klabu hiyo ili kutimiza malego yake.
“Nitaisaidia klabu yangu na kufanya vyote vinavyotakiwa ikiwa hata zaidi ya nilivyokuwa katika klabu yangu ya Yanga” amesema Ngassa.
Ngassa ameomba ushirikiano kwa wachezaji wengine ili kuifanikisha timu hiyo kufikisha malengo yake ya kuendelea kufanya vizuri.

Naye golikipa Chove amesema atafanya kila kuitumia nafasi hiyo aliyopewa kwani kuchaguliwa kwake na klabu hiyo kumekuwa kama bahati kwake kwani ni wengi walioiwania nafasi hiyo lakini wamekosa.
“Nimeipenda Azam FC tangu zamani, na kwa kuipata nafasi hii nitaitumani nitaafanya vizuri” amesema Chove golikipa wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Chove amewaomba wachezaji wengine wawape ushirikiano ili kufikia malengo yaliyowekwa na uongozi kwa kuwa katika namba mbili za juu.