VPL ROUND 26 HIGHLIGHTS | Mtibwa Sugar 0-1 Azam FC | April 28, 2018

Category: 

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya 26 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

Bao pekee la Azam FC limefungwa dakika ya 39 na mshambuliaji Shabaan Idd, aliyeunganisha kwa shuti mpira wa kona uliochongwa na winga Ramadhan Singano 'Messi', kona hiyo ilitokana na kipa wa Mtibwa, Shaaban Kado, kuipangua faulo nzuri iliyopigwa na nahodha msaidizi, Agrey Moris.

#TimuBoraBidhaaBora

#WavulanaWaChamazi

#SeasonOfRespect

#KataKiuYakoNaMajiSafiYaUhaiDrinkingWater

#NMBKaribuYako

#Tradegents

Back to Top