VIDEO: Kocha Azam FC akielezea michuano ya Azam Youth Cup U-13 (Juni 30, 2017)

Category: 

“Michuano ni mizuri mpaka sasa, inaelekea kwenye wiki ya tano (kesho), hivyo tumefikia kituo cha nusu ya mashindano, tunafurahia sana maendeleo, kwa wachezaji wetu wa Azam FC, kwenye wiki chache za mwanzo nadhani wachezaji walikuwa na presha na kushindwa kuonyesha uwezo wao, lakini kwa wiki mbili zilizopita walikuwa vizuri sana hasa wiki ya mwisho walipocheza na JMK Park Academy,” alisema Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, alipokuwa akizungumzia maendeleo ya kikosi chake kwenye michuano ya vijana Azam Youth Cup U-13.

Michuano hiyo itaendelea kesho Jumamosi kuanzia saa 3.00 asubuhi kwa mechi tatu; wenyeji Azam Academy U-13 wakikipiga na Bom Bom SC, JMK Park nao wataonyeshana kazi na Rendis huku Ilala Academy ikichuana na Magnet Youth.

Back to Top