Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC alivyozindua Azam Media Center leo

Category: 

OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Abdul Mohamed, leo amezindua chumba maalumu cha kufanyika mikutano ya waandishi habari (Media Center) chenye hadhi ya kimataifa kilichopo kwenye makao makuu ya timu hiyo Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Zoezi hilo limehudhuriwa na Mkuu wa KItengo cha Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas pamoja na yule wa Simba, Haji Manara, ambao waliipongeza timu hiyo kwa kuzidi kufanya mapinduzi kwenye soka la Tanzania.

Back to Top