CAF YAUMWAGIA SIFA UWANJA AZAM COMPLEX | May 22, 2018

Category: 

#AzamComplexInspections KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki leo mchana ilipokea ugeni kutoka kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) waliokuja kufanya ukaguzi wa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Uwanja huo umekaguliwa kutokana na kuwa moja ya viwanja vitakavyotumika kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri wa miaka 17 zitakazofanyika nchini mwakani.

Ugeni huo ulifika makao makuu ya Azam FC, wakiwa na wenyeji wao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye msafara akiwemo Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidau, ambao kwa kiasi kikubwa waliridhishwa na miundombinu ya uwanja huo.

Back to Top