KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeshindwa kusogea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kulazimishwa suluhu na Njombe Mji, mchezo uliomalizika usiku huu katika Uwanja wa Azam Complex.

Apr 15, 2018 10:40pm

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeshindwa kusogea hadi nafasi ya pili kwenye...

Apr 14, 2018 11:50am

HAIKUWA siku nzuri jana kwa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya kufungwa...

Apr 12, 2018 02:51pm

MVUA kubwa inayoendelea kunyesha Mlandizi mkoani Pwani imepelekea kuahirishwa kwa mchezo wa Ligi...

Apr 15, 2018 10:40pm

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeshindwa kusogea hadi nafasi ya pili kwenye...

Jul 23, 2013 10:31am

 

Majaribio kwa Azam Academy sasa yatafanyika Agosti 6 kuanzia saa moja asubuhi. Wazazi...

Jan 09, 2018 09:32pm

NAHODHA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, anaamini ya kuwa...

Jun 02, 2012 05:30am

Wakati wachezaji Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Erasto Nyoni, Waziri Salum,...

Jan 05, 2012 06:12pm

 

Nahodha Agrey Morris amewatoa shaka mashabiki wa Azam FC kwa kuhakikisha ushindi...

Apr 15, 2018 10:40pm

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeshindwa kusogea hadi nafasi ya pili kwenye...

Sep 13, 2014 04:08pm

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Joseph Marius Omog amesema kwamba kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa...

Jul 10, 2016 01:55pm

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, umetangaza rasmi kuwatema wachezaji...

Nov 11, 2016 10:25pm

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa...

News by Cetegory

Highlight News

Apr 15, 2018 10:40pm

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeshindwa kusogea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kulazimishwa suluhu na Njombe Mji, mchezo uliomalizika usiku huu katika Uwanja wa Azam Complex.

Ushindi wowote wa Azam FC leo ungeifanya kusogea hadi nafasi ya pili ikiishusha Yanga, ambayo ingerejea nafasi yake hiyo itakapopata matokeo mazuri kwenye mechi zake tatu za viporo.

Safu ya ushambuliaji ya Azam FC iliyokuwa...

Apr 14, 2018 11:50am

HAIKUWA siku nzuri jana kwa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Awali mchezo huo ilikuwa ufanyike juzi Alhamisi kabla ya kuahirishwa kufuatia mvua kubwa kunyesha mkoani humo na maji mengi kutwama kwenye sehemu ya kuchezea uwanjani hapo.

Azam FC imepoteza mchezo huo ikiwa kwenye vita kubwa ya kuhakikisha inamaliza...

Apr 12, 2018 02:51pm

MVUA kubwa inayoendelea kunyesha Mlandizi mkoani Pwani imepelekea kuahirishwa kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Azam FC.

Mchezo huo ulikuwa ufanyike leo saa 8.00 mchana kabla ya mvua hiyo kutibua baada ya kuanza kunyesha majira ya 7 mchana na kufanya Uwanja wa Mabatini kujaa maji kwenye eneo la kuchezea.

Baada ya mwamuzi wa mchezo huo, Shomari Lawi (Kigoma), kuzishirikisha timu zote mbili kwa kuukagua uwanja, walifikia uamuzi wa...

Apr 11, 2018 01:41pm

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, muda wowote kuanzia sasa itaanza safari ya kuelekea mkoani Pwani tayari kabisa kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Mabatini kesho Alhamisi saa 10.00 jioni.

Kikosi hicho kinaelekea huko na nyota wake 20, ambao watakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha wanasaka ushindi muhimu ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi hiyo, ambapo kwa sasa imejizolea pointi 45 katika...

Apr 08, 2018 08:06pm

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetoka suluhu dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliomalizika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo jioni.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 45 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa imebakia nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi nne na kinara Simba aliyenazo 49 na Yanga ikiwa imejikusanyia 46 katika nafasi ya pili, timu hizo mbili zikiwa na mechi mbili mkononi.

Azam...

Apr 07, 2018 10:48am

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakuwa kibaruani ugenini kutafuta pointi tatu muhimu pale itakapokuwa ikikabiliana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya kesho Jumapili saa 10.00 jioni.

Tayari kikosi cha Azam FC kimeshawasili mkoani humo jana usiku baada ya safari ndefu ya takribani saa 17 ikitokea jijini Dar es Salaam, ambapo imejidhatiti vilivyo kupata ushindi na leo jioni kitafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja huo.

Benchi la ufundi la...

Apr 05, 2018 07:51am

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuelekea mkoani Mbeya kesho Ijumaa alfajiri ikiwa imejidhatiti kuzoa pointi zote tatu itakapoivaa Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Sokoine, jijini Jumapili hii.

Azam FC inaelekea mkoani humo ikiwa na kumbukumbu ya kutolewa na Mtibwa Sugar kwenye Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) wikiendi iliyopita kwa mikwaju ya penalti 9-8 kufuatia dakika 90...

Apr 03, 2018 12:10am

BENCHI la Utabibu la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, limetoa ripoti ya maendeleo ya wachezaji wawili wa timu hiyo, mshambuliaji Wazir Junior na beki Daniel Amoah, waliopelekwa kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa matibabu.

Wakati Junior akiwa anasumbuliwa kwenye enka, Amoah kwa upande wake alikuwa akisikia maumivu kwenye goti, majeraha aliyopata miezi miwili iliyopita katika mchezo wa kirafiki wa Azam FC dhidi ya Polisi Tanzania...

Apr 01, 2018 12:19pm

BEKI wa Azam FC, David Mwantika, anaendelea vizuri baada ya kupata hitilafu ya mwili wakati wa mchezo wa wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sporst Federation Cup) dhidi ya Mtibwa Sugar usiku wa kuamkia leo.

Mwantika alipata tatizo hilo dakika ya 64 na kupatiwa matibabu ya awali kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mbagala Zakhem na kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, na baadaye ile ya Rufaa ya Muhimbili (MNH).

Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankema,...

Apr 01, 2018 10:35am

HAUKUWA usiku mzuri jana kwa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ikifungwa na Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penalti 9-8 kufuatia dakika 90 kumalizika kwa suluhu.

Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, ulikuwa ni mkali na wa aina yake, ambapo Azam FC itabidi ijilaumu baada ya kupoteza nafasi takribani nne za kufunga mabao dakika 30 za mwanzo za mtanange huo.

Matokeo hayo...

Mar 27, 2018 03:35pm

ZIMEBAKIA siku nne kabla ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, haikijavaana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii sa 1.00 usiku.

Wakati kikosi hicho kikienda kucheza na Mtibwa Sugar, leo tunaangalia rekodi za timu zote mbili kwenye mechi sita zilizopita za mashindano yote.

Azam FC inaonekana kuwa moto, baada ya kushinda mechi nne kati ya sita...

Mar 26, 2018 10:06am

BAADA ya kufunga mabao mawili kwenye mechi yake kwanza msimu huu, winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga, ameweka wazi kuwa atahakikisha anakuwa vizuri zaidi.

Kimwaga aliyekuwa nje ya dimba tokea Agosti 24 mwaka jana baada ya kupata majeraha ya goti kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu cha TTC cha mkoani Mtwara, wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda ulioisha kwa matajiri hao kushinda bao 1-0.

Mabao hayo mawili Kimwaga...

Back to Top