Wataalamu wa Afya waridhishwa na Uwanja wa Azam Complex

Category: 
Team: 
Azam FC

KLABU ya Azam leo imepokea ugeni mzito ulioongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam (RMO), Dkt. Rashid Seif Mfaume.

Dhumuni la ugeni huu lilikuwa kuangalia namna ambayo klabu yetu imejipanga kimiundombinu kuelekea kurejea kwa ligi kuu.

Ugeni huo ulijumuisha Afisa Afya Manispaa ya Temeke, Rehema Sadick,  Afisa Afya Manispaa ya Ilala, Reginald Mlay, pamoja na uongozi wa juu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA), ambapo Katibu Mkuu wake, Msanifu Kondo na Mkurugenzi wa Mashindano, Daudi Kanuti.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Dkt. Mfaume, ameelezea kuridhishwa na namba Azam FC ilivyojipanga.

"Nimeridhishwa sana na uwekezaji mlioufanya katika upande wa tahadhari dhidi ya virusi hatari vya corona.

Huu mtambo mlioufunga hapa ni wa aina yake, kwa kweli mnastahili kuwa mfano kwa viwanja vingine kama taifa na uhuru.

Jambo tunalopenda kusisitiza tu kuwa makini katika kuwakumbusha mashabiki wanaokuja hapa kuzingatia kuweka umbali (social distancing) baina yao.

Zaidi ya hapo, naomba niwaopengeze sana".

Meneja wa uwanja huo, Sikitu Kilakala, amesema klabu imekuwa ikifanya kila kitu kwa miongozo ya Serikali kupitia Wizara ya Afya, na iko tayari kuendelea kupokea maelekezo ili kuhakikisha watu wote wanaokuja uwanjani wanakuwa salama na kurudi majumbani kwao salama.

Back to Top