Error message

Deprecated function: The each() function is deprecated. This message will be suppressed on further calls in menu_set_active_trail() (line 2404 of /home/azam10/public_html/includes/menu.inc).

Azam FC v Kagera sasa kupigwa J4

Category: 
Team: 
Azam FC

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeufanyia marekebisho mchezo wa Azam FC dhidi ya Kagera Sugar, ambao sasa utapigwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Awali mchezo huo ulikuwa ufanyike Jumatano ijayo, lakini taarifa ilizotumiwa timu hiyo zinaeleza kuwa sasa umerudishwa nyuma siku moja na utafanyika Jumanne saa 10.00 jioni.

Kikosi cha Azam FC tayari kimewasili jijini humo tokea jana na leo asubuhi kilifanya mazoezi ya kwanza kwenye Uwanja wa Nyamagana, tayari kwa maandalizi ya mchezo huo.

Timu hizo zinakutana kwa mara ya pili mfululizo ndani ya siku tano, ambapo Ijumaa iliyopita zilicheza kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), Azam FC ikishinda bao 1-0 lililofungwa na winga Joseph Mahundi.

Lakini utakuwa ni mchezo wa tatu msimu huu kukutana, kwani zilishakutana kwenye raundi ya kwanza ya ligi, Azam FC ikashinda bao 1-0 katika Uwanja wa Kaitaba, bao lililofungwa na mshambuliaji Donald Ngoma.

Back to Top