Error message

Deprecated function: The each() function is deprecated. This message will be suppressed on further calls in menu_set_active_trail() (line 2404 of /home/azam10/public_html/includes/menu.inc).

Azam FC tayari ipo Shy kutifuana na Mwadui

Category: 
Team: 
Azam FC

KIKOSI cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, saa 8 usiku wa kuamkia leo kiliwasili salama mkoani Shinyanga tayari kabisa kwa mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Mwadui utakaofanyika Uwanja wa Mwadui Complex keshokutwa Ijumaa saa 8.00 mchana.

Azam FC kimewasili kikiwa na kikosi chake kamili isipokuwa kiungo mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu, atayeungana na timu muda wowote kaunzia sasa akitokea kwenye majukumu ya timu ya timu yake ya Taifa Zimbabwe.

Wachezaji wengine wa Azam FC ambao hawajaungana na timu ni mshambuliaji Wazir Junior pamoja na beki Yakubu Mohammed na Donald Ngoma, ambao wanaendelea na programu ya kujiweka fiti kabla ya kuanza kucheza mechi za ushindani wakitoka kwenye majeraha huku Joseph Kimwaga, akiwa majeruhi.

Mara baada ya kuwasili, kikosi hicho kinatarajia kufanya mazoezi leo Jumatano jioni kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa kabla ya kesho Alhamisi kujifua tena katika Uwanja wa Mwadui itakaochezea mchezo huo, unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake.

Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha juisi cha African Fruti, maji safi ya Uhai Drinking Water na Tradegents Tanzania Limited, hadi sasa inashika nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na pointi sita ikishinda mechi mbili za awali ilizocheza, ikizidiwa pointi moja na Mbao inayoongoza kileleni ikiwa na pointi saba lakini ikicheza mechi moja zaidi.

Back to Top