Azam FC kujipima vs Transit Camp

Category: 
Team: 
Azam FC

BAADA ya kufanya mazoezi kwa wiki moja, kikosi cha Azam FC kinatarajia kujipima nguvu dhidi ya Transit Camp inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Mchezo huo wa kirafiki unatarajia kufanyika Uwanja wa Azam Complex keshokutwa Jumamosi saa 1.00 usiku.

Benchi la ufundi la Azam FC litautumia mchezo huo, kuwaangalia wachezaji wake namna walivyopokea mafunzo kwa kipindi chote cha wiki moja walichofanya mazoezi.

Azam FC inaendelea na mazoezi yake kujiandaa na mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, ikitarajiwa kucheza dhidi ya Simba kwenye robo fainali.

Aidha imepangwa kuanza na Mbao Juni 14 mwaka huu kwenye urejeo wa ligi hiyo, iliyosimamishwa kwa muda wa miezi miwili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).

Tayari wachezaji wote wamesharipoti kambini, isipokuwa wachezaji saba wa kimataifa, ambao wanasubiria mipaka ya nchi zao ifunguliwe, ambao ni kipa Razack Abalora, mabeki Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, kiungo mshambuliaji Never Tigere na mshambuliaji Donald Ngoma.

Back to Top