Azam FC kuendeshwa kiuweledi zaidi

Category: 
Team: 
Azam FC

UONGOZI wa Klabu ya Azam unaendelea na mchakato wa kufanikisha uendeshaji wa timu katika misingi ya kiuweledi.

Mchakato huo unaratibiwa na Wakufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na Afrika (CAF), Dr. Henry Tandau (Utawala, FIFA) na Sunday Kayuni (Makocha, CAF).

Wakufunzi hao jana Alhamisi, waliwasilisha uchambuzi wa mchakato huo, mara baada ya kufanya tathimini ya awali, iliyohusisha mahojiano yao binafsi waliofanya na wachezaji, makocha, wafanyakazi na watu wa karibu na eneo la makao makuu ya klabu, Azam Complex.

Mara baada ya kuwasilisha uchambuzi huo, wakufunzi hao wataandaa mafunzo kwa idara mbalimbali ndani ya timu hiyo kuanzia kwenye uongozi, wafanyakazi, makocha, wachezaji na idara ya habari.

Aidha baada ya mafunzo hayo, mchakato huo utahitimishwa na utekelezaji wa kila idara katika shughuli zao za kila siku za klabu, wakitakiwa kuhakikisha wanatimiza kiuweledi yale yote waliyofundishwa.

#WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora

Back to Top