ASFC Robo Fainali | Ni Simba SC v Azam FC

Category: 
Team: 
Azam FC

TIMU ya Azam FC imepangwa kucheza na Simba katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Mchezo huo unatarajia kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Juni 27 na 28 mwaka huu.

Droo hiyo imefanyika leo Ijumaa kwenye ofisi za wadhamini wa michuano hiyo, Azam Media.

Azam FC ikipenya raundi hiyo, kwenye nusu fainali itakutana na mshindi wa robo fainali nyingine kati ya Yanga na Kagera Sugar.

Mechi nyingine za robo fainali itazikutanisha, Namungo dhidi ya Alliance huku Sahare All Stars ikichuana na Ndanda, na washindi wawili wa hizo mechi watakutana katika nusu fainali.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Bahati Vivier, akizungumzia droo hiyo alisema mechi itakuwa ngumu, lakini watajipanga kuhakikisha wanasonga mbele.

“Sisi tutajaribu kufanya mazuri ili tuwatoe ili tuone kama tunaweza kuendelea safari yetu nina imani kama tutajiweka vizuri kama benchi la ufundi tutatayarisha timu yetu kwa kuiweka salama na kuwa tayari kutafuta ushindi kwa hiyo mechi ili tuione nusu fainali,” alisema.

Azam FC ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo, na kuhusu hilo Vivier ameweka wazi kuwa wanachohitaji ni kushika nafasi ya kwanza kwa kuchukua tena taji hilo.

Back to Top